navigation

WASHINDI WA PAMWARDS 2009 WAREJEA NCHINI. 4 février, 2011

Posté par nyotayamsanii dans : Non classé , trackback

riziki.jpgWasanii wawili kati ya 3 walioshinda tuzo la Pearl of Music Awards, PAMWARD’S msimu wa 2009 wamerejea nchini baada ya ziara iliowafikisha Kigali Rwanda, Kampala Uganda na Dar es Salam Tanzania. wasanii hao ni pamoja na Steven Sogo pamoja na Riziki. wakizungumza na vyombo vya habari alhamisi hii Februari 3, wamesema kunufaika na ziara hiyo ambayo ilikuwa na dhamira ya kutangaza nyimbo zao. wamewashukuru waandalizi wa PAMAWARD’S ambao ni kutoka shirika la Menya Media. Wakiwa katika nchi hizo 3 walizo zitembelea, wamesema walitembelea vituo vingi vya redio na Televisheni za nchi hizo, na kupokelewa vema, hata nyimbo zao wamesema zilipokelewa vizuri na wananchi, kwani katika baadhi ya vipindi walivyo vifanya nyimbo zao zilichezwa hukui wananchi wakishiriki kupitia njia ya simu na kuomba zichezwe tena. Kuhusu kundi la Lion Story ambalo lilishinda pia taji hilo la PAMAWARD’S, Excellent Nimubona anaehusika na mawasiliano kwenye shirika la Menya Media alisema kwamba vijana wa kundi hilo walikataa kusafiri mmoja aidha wawili, walipenda wasafiri kundi nzima, jambo ambalo halingeli wezekana, kwani walikuwa wamekwenda kutangaza nyimbo na sio kupiga muziki. Riziki na Steven Sogho wamewatolea mwito wasanii wengine kutodharau michuano ya aina yoyote ile, kwani manufaa walioyapata yanazidi hata dhamani ya kupewa pesa.

Commentaires»

pas encore de commentaires

Laisser un commentaire

toutstar |
association des coeurs alliés |
Firmennetzwerk |
Unblog.fr | Créer un blog | Annuaire | Signaler un abus | twitocce
| aka7
| draria