navigation

D.ROP ARUDI TENA 4 février, 2011

Posté par nyotayamsanii dans : Non classé , ajouter un commentaire

drop.jpgMmoja kati ya wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Wakali Power D.Rpop asema sasa anarejea tena kwenye game baada ya kukosekana jukwaani kwa muda. Msanii huyo wa miondoko ya kufokafoko ama hip hop, amesema kwamba ameona mengi na amejifunga mengi katika safari yake alioifanya huko Dar es salama Tanzania. tangu kurejea nchini tayari amekwisha recordi nyimbo 3 aliuzoimba mwenyewe. aliskika akisema kwamba wapenzi wa muziki nchini Burundi watasikia mengi na wataona mabadiliko mengi mwaka huu kutoka kwake, kwani amekuja kivingine.

WASHINDI WA PAMWARDS 2009 WAREJEA NCHINI.

Posté par nyotayamsanii dans : Non classé , ajouter un commentaire

riziki.jpgWasanii wawili kati ya 3 walioshinda tuzo la Pearl of Music Awards, PAMWARD’S msimu wa 2009 wamerejea nchini baada ya ziara iliowafikisha Kigali Rwanda, Kampala Uganda na Dar es Salam Tanzania. wasanii hao ni pamoja na Steven Sogo pamoja na Riziki. wakizungumza na vyombo vya habari alhamisi hii Februari 3, wamesema kunufaika na ziara hiyo ambayo ilikuwa na dhamira ya kutangaza nyimbo zao. wamewashukuru waandalizi wa PAMAWARD’S ambao ni kutoka shirika la Menya Media. Wakiwa katika nchi hizo 3 walizo zitembelea, wamesema walitembelea vituo vingi vya redio na Televisheni za nchi hizo, na kupokelewa vema, hata nyimbo zao wamesema zilipokelewa vizuri na wananchi, kwani katika baadhi ya vipindi walivyo vifanya nyimbo zao zilichezwa hukui wananchi wakishiriki kupitia njia ya simu na kuomba zichezwe tena. Kuhusu kundi la Lion Story ambalo lilishinda pia taji hilo la PAMAWARD’S, Excellent Nimubona anaehusika na mawasiliano kwenye shirika la Menya Media alisema kwamba vijana wa kundi hilo walikataa kusafiri mmoja aidha wawili, walipenda wasafiri kundi nzima, jambo ambalo halingeli wezekana, kwani walikuwa wamekwenda kutangaza nyimbo na sio kupiga muziki. Riziki na Steven Sogho wamewatolea mwito wasanii wengine kutodharau michuano ya aina yoyote ile, kwani manufaa walioyapata yanazidi hata dhamani ya kupewa pesa.

BIGSAME

Posté par nyotayamsanii dans : Non classé , ajouter un commentaire

HuyuBIGSAME ni mmoja kati ya waazilishi wa studio zaku record jijini Bujubmuura, baada ya studio maarufu sana miaka ya 2000, ijulikanayo kama Menye Media Studio,  Bigmase Studio pia ni miongoni mwa Studio za mwanzo mwanzo kabisa jijini Bujumbura, inapatikana tarafani Buyenzi na mmiliki wake ni Salum a.k.a Bigsame. Studio hiyo inapatikana tarafani Buyenzi

Bonjour tout le monde ! Hamjambo nyote

Posté par nyotayamsanii dans : Non classé , ajouter un commentaire

Ni matumaini yangu kwamba upo salama salimi popote unapo nisoma ma wakati huu. Hii ni sehemu maalum ambayo utazipata habari za wasanii wmbalimbali hususa wasanii wa Burundi. Ukitaka kuwatambua, tembelea safa hii.

Karibu,

Muhariri
 

toutstar |
association des coeurs alliés |
Firmennetzwerk |
Unblog.fr | Annuaire | Signaler un abus | twitocce
| aka7
| draria